28 Julai 2016 - 10:59
Serikali ya Uturuki yavifungia vyombo vya habari

Serikali ya Uturuki imeamuru kufungwa kwa vyombo kadhaa vya habari yakiwemo mashirika ya habari, vituo vya matangazo kwa njia ya televisheni na radio pamoja na magazeti.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Uturuki imeamuru  kufungwa kwa vyombo kadhaa vya habari  yakiwemo mashirika ya habari, vituo vya matangazo kwa njia ya televisheni na  radio  pamoja na magazeti. Serikali ya nchi hiyo pia imetoa waranti wa kukamatwa kwa waandishi kadhaa wa habari  ikiwa ni sehemu ya operesheni inayoendelea ya kuwatia mbaroni watu wanaoshukiwa na kuhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa  la Julai 15, mwaka huu.  Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim  hapo jana ameonya kuwa operesheni hiyo haijafika mwisho kutokana na serikali ya nchi hiyo kutoa waranti wa kukamatwa kwa wafanyakazi kadhaa wazamani wa  magazeti.  Zaidi ya watu  15,000 tayari wametiwa mbaroni wakihusishwa na jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa.

Serikali ya Uturuki imehusishwa na mauaji  ya kinyama dhidi ya watuhumiwa wanaoshukiwa kushiriki mapinduzi hayo.

Mwisho wa habari/ 291